Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 17 wateketea kwa moto nchini Kenya

Wanafunzi 17 Wateketea Kwa Moto Nchini Kenya.png Wanafunzi 17 wateketea kwa moto nchini Kenya

Fri, 6 Sep 2024 Chanzo: Bbc

Wanafunzi kumi na saba wateketea kwa moto hadi kutoweza kutambulika katika ajali ya moto iliyotokea kwenye shule ya Hillside Endarasha iliyopo kaunti ya Nyeri nchini Kenya.

Akithibitisha kisa hicho, msemaji wa polisi nchini Kenya Dr. Resila Onyango amesema kwamba maafisa wa polisi wa kuchunguza jinai wamefika katika shule hiyo kuanza uchunguzi wa kilichochangia moto huo.

14 wanapata matibabu katika hospitali mbali mbali katika kaunti hiyo ya Nyeri iliyopo katika eneo la kati mwa nchi hiyo.

Kwa sasa shule imefungwa huku polisi wakichunguza bweni ambapo moto huo ulianza.

Rais wa Kenya William Ruto ametoa salamu za pole kwa Wakenya.

Amesema Serikali inakusanya rasilimali zote muhimu ili kusaidia familia zilizoathiriwa.

Chanzo: Bbc