Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokufa kwa maporomoko ya udongo Ethiopia wapindukia 150

Maporomoko Ethiopiaaaaaaaa.jpeg Waliokufa kwa maporomoko ya udongo Ethiopia wapindukia 150

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya watu walioaga dunia katika maporomoko ya udongo yaliyoikumba Ethiopia baada ya mvua kubwa kunyesha nchini humo inazidi kuongezeka ambapo takwimu za karibuni zinaonyesha kuwa imepindukia 150.

Maporomoko ya udongo, majanga ya kimaumbile ya msimu nchini Ethiopia yamesababisha vifo vya takriban watu 157, huku majeruhi haswa wakiwa hawajulikani waliko kwa sababu watu wengi hawajulikani waliko baada ya maporomoko mengine makubwa kuwafunika watu waliokuwa wakijaribu kuwaokoa wengine.

Wengi wa wahanga waliuawa walipokuwa wakijaribu kuwaokoa manusura wa maporomoko ya udongo hapo awali.

Maporomoko ya ardhi ni ya kawaida wakati wa msimu wa mvua nchini Ethiopia, ambao ulianza Julai na unatarajiwa kudumu hadi katikati ya Septemba.

Markos Melese Mkurugenzi wa Wakala wa Kukabiliana na Maafa katika Kanda ya Gofa amesema kuwa, hadi sasa watu wengi hawajulikani walipo miongoni mwa kundi hilo lililofukiwa na matope wakati wakijaribu kuwanusuru watu.

Operesheni za kutoa misaada ziliendelea Jumatano ya jana, saa 48 baada ya maporomoko hayo ya ardhi ambayo yalisababisha vifo vya karibu watu 230 katika eneo la pekee la kusini mwa Ethiopia, ambapo wasaidizi wa kibinadamu wanatoa misaada na watu 14,000 wanatakiwa waondolewe haraka.

Kulingana na Firaol Bekele, mkurugenzi wa Kitengo cha Tahadhari ya Mapema katika Tume ya Kudhibiti Hatari ya Maafa ya Ethiopia (EDRMC) ni kuwa, shughuli za utafutaji zimeimarishwa na "ndege zisizo na rubani zinazoendeshwa na wataalamu kutoka INSA", shirika la usalama mtandaoni la Ethiopia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live