Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliodaiwa kuwa na Corona Sierra Leone, wakutwa Negative

BEA53FF6 7FFB 440F BD4F CD61F4A347B9 660x400.jpeg Waliodaiwa kuwa na Corona Sierra Leone, wakutwa Negative

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Wachezaji watano wa Timu ya Taifa Benin waliosababisha mchezo kati yao na Sierra Leone jana kuahirishwa kwa kuwa na maambukizi ya Corona leo wamepimwa Aiport na kukutwa Negative.

Benin jana waligoma kucheza dhidi ya Sierra Leone baada ya kudai kuwa Sierra Leone imefoji matokeo ya Corona ya wachezaji hao ili wakosekane katika mchezo na Sierra Leone ipate matokeo, mchezo huo uliahirishwa hadi mwezi Juni.

Hii imekuwa ni tamaduni ya timu mwenyeji kutumia kigezo cha Corona kudhoofisha timu mgeni katika soka la Afrika, Uganda wakiwa Malawi walikutana na Changamoto hii ila baada ya mvutano na FA ya Malawi baadae wakawaruhusu wachezaji wao wacheze.

Hata hivyo Sierra Leone inapinga mchezo huo kuahirishwa na sasa wanataka wazadiwe point tatu za mezani kwa kutumia kigezo kuwa Benin waligoma kucheza mchezo huo.

Chanzo: millardayo.com