Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya waungana kupinga mfumuko wa bei za bidhaa

Kenya Uchumi Wakenya waungana kupinga mfumuko wa bei za bidhaa

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara pamoja na kaya za nchini Kenya wanaungana na raia wawili waliofungua mashtaka katika Mahakama kuu ya nchini humo kupinga ongezeko la kodi la kila mwaka jambo ambalo limepelekea mfumuko wa bei wa asilimia 4.97 sambamba na kupanda kwa bei mafuta inayotarajiwa kuanza mwezi Oktoba.

Ongezeko hilo la kodi limewekwa kwenye bidhaa zisizopungua 31 ikiwa ni pamoja na Juisi za matunda, maji ya chupa, bia, tumbaku, hali iliyopelekea maisha ya wananchi kuwa magumu zaidi.

Ugumu wa maisha katika taifa hilo umeongeza kufuatia kuongezwa kwa kodi hizo hali iliyopelekea kushuka kwa thamani ya shilingi nchini humo.

"Matokeo ya kupanda kwa bei kila mara yanaathiri uchumi wa nchi, gharama hazishihiki chakula kipo juu, usafirishaji wabidhaa upo juu, gharma ni kuba" amesema Katibu Mkuu wa wa Shirikisho la wanunuzi nchini humo.

Wiki iliyopita, taarifa ilitolewa na Seneti ikieleza kuongezeka kwa bei ya mafuta nchini jambo ambalo linapigiwa kelele na wananchi wakidai kuongezeka kwa ugumu wa maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live