Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waishtaki Serikali kupanda kwa Mafuta Kenya

Tozo Mafuta Ya Gari Waishtaki Serikali kisa kupanda kwa mafuta

Tue, 21 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raia wawili wa nchini Kenya, waliotambulika kwa majina ya Isaiah Odando na Wilson Yata,wamefungua mashtaka Mahakamani kuhusu kupanda kwa bei za mafuta kwa madai ya kuwa hazijazingatia hali ya mwananchi wa kawaida.

Wawili hao wamesema kuwa, serikali imepandisha bei ya mafuta pasipo kuwashirikisha wananchi huku kukiwa na ongezeko kubwa la kodi katika bidhaa nyingi nchini humo hali ambayo inaweka mzigo mkubwa kwa watumiaji na wananchi kwa ujumla.

Wameitaka Mamalaka ya Mapato ya Kenya (KRA) ilirekebisha tozo hizo zilizowekwa kwenye mafuta ambazo zinatarajiwa kuanza kutumika Oktoba 1, 2021 ikipitishwa na Bunge na Hazina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live