Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara wa samaki Kenya wakwama mpaka wa Uganda

Kenya Fish (600 X 337) Wafanyabiashara wa samaki Kenya wakwama mpaka wa Uganda

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanya biashara wa Samaki nchini Kenya wamesema kuwa wamekwama kusafirisha jumla ya tani 300 za samaki kwenda nchini Uganda kufuatia mzozo wa kibiashara unaoendelea baina ya mataifa hayo mawili.

Mapema mwezi Oktoba maafisa wa kitengo cha ulinzi na uvuvi FPU, kutoka katika mpaka wa Kasese uliopo Uganda walikamata malori matano ya samaki kutoka Kenya yaliyokuwa yakielekea nchini Congo.

Wafanyabiashara hao wamelalamikia mzozo huo kuwakwamisha kibiashara kwani wateja wao wakuu wanategemea mpaka wa Uganda ambao kwa sasa unakabiliwa na vuta ni kuvute za kibiashara baina ya mataifa hayo mawili.

"Kila wiki huwa nasafirisha tani 12 za samaki lakini kwa sasa nina zaidi ya wiki mbili sijafanikisha kusafirisha chohote kwenda Cngo kwasababu sina uhakika na usalama wa bidhaa zangu kufuatia mzozo huu unaoendelea" Ameema bwana Hassan Ahmad mfanyabiashra wa samaki Kenya.

Aidha wamesema kuwa hadi sasa hawafahamu kama tani hizo 300 zitasafirishwa ama la.

Mzozo wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili unaendelea kukomaa kila kukicha, mwanzo kulishuhudiwa kuwepo kwa sintofahamu ya maziwa ya Uganda yaliyokuwa yakisafirishwa kuelekea Kenya ambako ndiko kwenye soko kuu kuwekewa vizuizi vingi kwenye kodi jambo lililopelekea kuzorota kwa biashara hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live