Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji watano Eritrea watoweka kambini Uganda

Eritrea U20 Women Kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanawake Eritrea, Chini ya miaka 20

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetoa taarifa kwenye vyombo vya usalama vya Uganda juu ya kupotea kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Eritrea inayoendelea na mashindano CECAFA U20 kwa wanawake inayoendelea Jinja nchini Uganda.

Wachezaji hao mara ya mwisho walikuwa kwenye hoteli waliyofikia mjini Jinja ambapo Cecafa kwa kushirikiana na Polisi wa Jinja tayari wameanza upelelezi.

Hii siyo mara ya kwanza kwa wachezaji wa nchi za Eritrea, Somalia na Djibouti kupotea kwenye mashindano hayo yanayoshirikisha nchi za CECAFA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live