Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji Stars wapewa dakika 20 pekee

Starss Pic Data Wachezaji Stars wapewa dakika 20 pekee

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeshauriwa kuhakikisha inatumia vyema dakika 20 za mwanzo za mchezo kwa ajili ya kuwasoma wapinzani katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Equatorial Guinea. Taifa Stars inashuka dimbani kesho, kukabiliana na Equatorial Guinea mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara nyingine tena baada ya kushiriki mwaka 1980 na 2019. Mwanandinga wa zamani Chambua Sekilojo ameiambia Mwanaspoti leo kuwa, ili Stars iweze kufanya vizuri katika mchezo huo na kusonga mbele inatakiwa kutumia vyema dakika 20 za mwanzo wa mchezo kuwasoma wapinzani wao. Chambua amesema, ushindi wa Stars ni baada ya kucheza kwa nidhamu na kuheshimu mchezo huo kwa kutambua hilo watafanya vizuri na kusonga mbele.

"Kwanza nawaomba wachezaji waondoe kabisa hofu, wawaheshimu tu wapinzani basi hayo mengine ni matokeo, wakishatumia dakika 20 za kuwasoma watacheza vizuri tu," amesema. Aidha Sekilojo amewataka Watanzania kuwa na imani na kikosi kitakachopangwa kwani kila mchezaji aliyeitwa ndani ya kikosi hicho ana uwezo wa kufanya vizuri. Michezo ya kuwania kufuzu AFCON inatarajiwa kuanza kurindima hii leo ambapo Uganda itakuwa mwenyeji wa Burkina Faso, Sudan Kusini wakiumana na Malawi, Rwanda dhidi ya Mozambique, Ethiopia na Madagascar, Suinea dhidi ya Mali huku Sao Tome wakiwavaa Sudan.

Huku mechi za kesho

Comoro vs Togo

Afrika Kusini vs Ghana

Kenya vs Egypt

Gabon vs Congo

Gambia vs Angola

Botswana vs Zimbabwe

Zambia vs Algeria

Libya vs Tunisia.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz