Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge watatu wa upinzani wakamatwa Uganda

Bobi Wine Akamatwa Na Usalama Uwanja Wa Ent Wabunge watatu wa upinzani wakamatwa Uganda

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wabunge watatu wa Upinzani nchini Uganda waliwekwa kizuizini kabla ya kusikilizwa kwa kesi, Polisi walitangaza jana jioni katika mkesha wa maandamano dhidi ya ufisadi.

Walishtakiwa kwa makosa mbalimbali na kuwekwa kizuizini kabla ya kusikilizwa kwa kesi,” Msemaji wa Polisi wa Uganda aliambia AFP, akiongeza kuwa wote watapelekwa Mahakamani siku ya Alhamisi ijayo.

Wakati huo huo, Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine anasema vikosi vya usalama vilizingira makao makuu ya chama chake siku ya Jumatatu, mkesha wa maandamano yaliyopangwa ya kupinga ufisadi ambayo yalipigwa marufuku na mamlaka.

Bobi Wine, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba makao makuu ya chama chake, National Unity Platform (NUP), huko Kavule, kitongoji cha mji mkuu wa Uganda Kampala, yamezingirwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live