Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wababe wa Simba warejea Ligi ya Mabingwa Afrika

Jwaneng 342.jpeg Wababe wa Simba warejea Ligi ya Mabingwa Afrika

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Jwaneng Galaxy FC kutoka Botswana imerejea tena kwenye michuano ya klabu Bingwa Afrika (CAFCL) baada ya siku ya leo kutwaa ubingwa ligi ya Botswana kwa kuichapa Holy Ghost FC goli 2-0 na kufikisha alama 69, wakifatiwa na Gaborone United wenye alama 64.

Jwaneng galaxy ndio timu iliyoiondosha Simba kwenye michuano ya klabu Bingwa msimu wa 2021/22 baada ya Simba kupata ushindi wa goli 2-0 ugenini na baadae kukubali kichapo cha goli 3-1 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa (Agregate 3-3) na Simba kushuka hadi kombe la shirikisho kutokana na sheria ya goli la ugenini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live