Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WB yahimiza Afrika kuongeza kasi ya chanjo kuokoa uchumi

4a6e94dffe51518d235d58612eb793cf.jpeg BENKI ya Dunia (WB)

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BENKI ya Dunia (WB) imezihimiza nchi za Afrika kuongeza kasi ya matumizi ya chanjo ya Covid-19 ili kuokoa uchumi wao kutokana na athari za ugonjwa huo.

Hayo yalibainishwa na Mchumi Mkuu wa Benki hiyo barani Afrika, Albert Zeufack, kwenye mahojiano maalumu na Mtetezi wa Vijana wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef), Cynthia Nyongesa, kwa njia ya mtandao jana.

Alisema uharibifu wa uchumi uliosababishwa na janga hilo unatarajia kudumu kwa muda mrefu na kutokana na kasi ya ugonjwa huo kwa sasa, nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara nazo zitachukua muda mrefu kurejea katika hali yake ya kawaida iliyokuwepo kabla ya kuzuka kwa Covid-19

"Upatikanaji wa chanjo yenye ufanisi na salama ya Covid-19 ni muhimu katika kuokoa maisha na kuimarisha urejesho wa uchumi wa Afrika. Kupelekwa kwa chanjo kwa haraka kutaongeza kasi ya ukuaji wa uchimi wa Bara hilo kufikia asilimia 5.1 mwaka 2022 na asilimia 5.4 mwaka 2023 kama hatua zaidi za kuzuia corona zitachukuliwa pamoja na kuongeza matumizi na uwekezaji," alisema Zeufack.

Alisema makisio ya ukuaji wa uchumi Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa mwaka 2022 ni asilimia 3.5 na utarajiwa kukua kwa asilimia 3.8 mwaka 2023 na mpaka mwisho wa mwaka huu ukuaji unatarajiwa kufikia asilimia 3.3.

Kwa mujibu wa Zeufack, kama Afrika itaongeza kasi ya matumizi ya chanjo ya Covid-19, ukuaji huo unaweza kuwa wa haraka hadi kufikia asilimia tano mwaka 2022 na asilimia 5.4 mwaka 2023.

Alisema nchi zenye uchumi mkubwa Afrika ikiwemo Angola, Nigeria na Afrika Kusini zinatarajiwa kukua kwa asilimia 0.4, asilimia 2.4 na asilimia 4.6 mtawalia.

Kuhusu mabadiliko ya tabianchi, Zeufack alisema kuwa nchi za Afrika hazina budi kuhakikisha kuwa mabadiliko ya tabianchi yanakuwa sehemu ya utungwaji wa sera za kiuchumi barani humo.

Alisema japo Afrika inachangia chini ya asilimia nne ya uzalishaji wa hewa ukaa, bado inaathirika na madhara ya mabadiliko ya tabianchi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz