Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viwanda 30 vya vyakula vyafungwa nchini Kenya

Kenya Picsd Viwanda 30 vya vyakula vyafungwa nchini Kenya

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wazalishaji thelathini wa chakula cha mifugo nchini Kenya wamelazimika kufunga viwanda vyao kwa muda wa miezi miwili sasa kufuatia uhaba wa malighafi pamoja na kupungua kwa uhitaji wa vyakula hivyo katika masoko mengi.

Taarifa hii imetolewa na Chama cha Watengenazaji wa Chakula Kenya (AKEFEMA) na kusema kuwa viwanda hivyo vimekabiliwa na usambazaji hafifu hasa kwa bidhaa kama za soya na alizeti ambazo bei zake zimeongezeka mara mbili baada ya marufuku mpya ya kusafirisha bidhaa hizo kutolewa katika nchi ya Zambia ambao ndio wateja wao wakuu.

Uhaba wa bidhaa hizi umepelekea kuongeza kwa bei za vyakula, ambapo kilo 50 za unga sasa zinauzwa kwa Ksh 2850 sawa na Tsh 59,800 kutoka kuuzwa Ksh 2750 sawa na 57,700 wiki iliyopita.

Hata hivyo inaelezwa kuwa kampuni 15 kati ya 30 zilifungwa mwezi wa nane hali ambayo imechochea kwa kasi mfumko mkubwa bei za bidhaa .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live