Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Vikwazo havitatuondoa kwenye vita' – Mkuu wa waasi DRC

Drc Amnestyyyyy 'Vikwazo havitatuondoa kwenye vita' – Mkuu wa waasi DRC

Fri, 26 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa muungano wa muungano wa waasi wa DRC wa Alliance Fleuve Congo (AFC) unaojumuisha kundi la M23, Corneille Nangaa, amesema kwamba vikwazo vya Marekani havitawazuia katika mapambano yao ya "kuirejesha uthabiti wa nchi " na kusema: "lengo ni Kinshasa, tutafika huko".

Siku ya Alhamisi, Ofisi ya udhibiti wa mali za kigeni katika wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza kuwa serikali ya Marekani imewawekea vikwazo viongozi watatu wa makundi yenye silaha mashariki mwa Congo.

Waliowekewa vikwazo hivyo ni Corneille Nangaa, mkuu wa AFC, Bertrand Bisimwa, mkuu wa kitengo cha siasa katika M23, na Kanali Charles Sematama, mmoja wa viongozi wa kundi la Twirwaneho(Tujipiganie), linaloendesha harakati zake katika jimbo la Kivu Kusini.

Serikali ya Marekani inashutumu watatu hao kwa kuchangia vita, ghasia, na kuwadhuru raia "ili kufikia malengo yao ya kisiasa".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live