Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vihiga Queens waibuka kidedea kombe la Samia

Vihiga Queens Vihiga Queens wakishangilia Ubingwa

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji wa mashindano ya kufuzu fainali za Afrika za Wanawake, Vihiga Queens imetwaa ubingwa wa Kombe la Samia Cecafa kwa kuifunga Commercial Bank of Ethiopia (CBE) kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Kasarani, Nairobi Kenya.

CBE ambao walikuwa hawajafungwa mpaka walipofuzu fainali waliifunga Lady Doves kwa penalti 5-3 baada ya kumaliza dakika 120 kwa sare ya 1-1 na Vihiga Queens waliifunga Simba Queens kwa mabao 2-1 katika mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Simba Queens ya Tanzania bara imeshika nafasi ya nne baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Lady Doves ya Uganda katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliochezwa mapema mchana.

Kwa matokeo hayo bingwa Vihiga Queens imeondoka na zawadi ya kombe na Dola za Marekani 30,000, CBE ikaondoka na 20,000 na Lady Doves ikaambulia 10,000 lakini pia zilikuwepo zawadi za mchezaji mmoja mmoja ambapo mfungaji bora ni Geinore Loza Abera wa CBE aliyepachika mabao 13.

Katibu Mkuu wa FIFA Fatma Samoura, ndiye alikuwa mgeni wa heshima katika fainali hizo akifuatana na ofisa wa soka la wanawake wa FIFA, Sarai Bareman.

Mpaka wanafika Fainali wenyeji hao hawakuwahi kupoteza mchezo zaidi ya kutoa suluhu ya bila kufungana na Timu ya Simba Queens katika hatua za makundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live