Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vera Sidika ajiandaa kuondoka hospitalini baada ya kujifungua

Ae1c5509a92cf248 Vera Sidika ajiandaa kuondoka hospitalini baada ya kujifungua

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Sosholaiti Vera Sidika alijifungua mtoto wake wa kwanza Oktoba 20 na kumpa jina Asia BrownVera amekuwa akiwajuza mashabiki wake kila tukio linalojiri tangu alipopata ujauzito hadi siku aliyojifungua.

Mrembo huyo ambaye alijifungua kupitia njia ya upasuaji, alisema kwamba hakuhisi uchungu wowote, madai yaliyoibua hisia tofauti miongoni mwa akina mama. Sosholaiti na mfanyabiashara maarufu Vera Sidika aliposti video kwenye mtandao wa Instagram iliyomuonyesha akihudumiwa na muuguzi huku akiwa anajiandaa kuondoka hospitalini.

Vera na mumewe Brown Mauzo walijaliwa mtoto wao wa kwanza siku ya Jumanne, Oktoba 20 na kumpa jina Asia Brown.

Kupitia kwenye video yake ya hivi punde, Vera alilimbikizia sifa chungu nzima mumewe na kumshukuru kwa kusimama naye tangu alipoanza safari ya ujauzito hadi alipojifungua malaika wao.

"Tunapojiandaa kuelekea nyumbani na @princess_asiabrown, ningependa sana kumshukuru mpenzi wangu @brownmauzo254 kwa kusimama nami, najihisi mkamilifu sasa" Vera aliandika Instagram.

Awali, Vera aliibua hisia mseto mitandaoni baada ya kudai kwamba hakuhisi uchungu wowote wakati alifanyiwa upasuaji na kwamba yuko tayari kupata watoto wengine kwa mpigo.

Kabla ya kujifungua, Vera alikuwa amesema kwamba atajipaka vipodozi wakati wa kuingia thieta kufanyiwa upasuaji wa kujifungua mwanawe ambaye alipata mashabiki zaidi ya 5,000 mitandani dakika 30 baada ya kuzaliwa.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke