Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzalishaji zao la chai Kenya wapungua kwa kilo milioni 26

AAOTJa9dd.jfif Uzalishaji zao la chai Kenya wapungua kwa kilo milioni 26

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uzalishaji wa zao la chai nchini kenya unatajwa kupungua kwa zaidi ya kilo milioni 26 katika miezi sita ya mwanzo wa mwaka 2020 kufuatia hali mbaya ya hewa katika maeneo linapolimwa zao hilo.

Bodi ya Chai imetoa taarifa hii na kusema kuwa katika miezi hiyo waliweza kuzalisha jumla ya kilo milioni 274 za chai tofauti na miezi iliyofuata ambayo walizalisha kilo milioni 300 kwa mwaka huo huo.

Hali hii imesababishwa na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa katika maeneo mengi ya nchini humo, ikiwa ni pamoja na ukame na baridi kali ambavyo vyote vimeathiri ukuaji wa zao hilo.

"Kwa sababu ya hali mbaya ya hali ya hewa mwaka huu , pamoja na athari za joto na baridi ambazo zinatarajiwa kuendelea hadi mwisho wa mwezi Agosti na kufuatiwa na vipindi vya joto kali hadi Oktoba, uzalishaji wa zao hili unatarajiwa kuendelea kuwa chini zaidi" imesema taarifa ya Bodi hiyo.

Hata hivyo kumeripotiwa kuwepo kwa ongezeko kubwa la usafirishaji wa chai mara baada ya wafanyabiashara wa zao hilo kutoa malighafi walizokuwa wameziweka ghalani.

Inaelezwa kuwa usafirishaji huo umeongeza kwa aslimia 19 kulinganisha na vipindi vilivyopita, kwa kusafirisha kilo milioni 298 kutoka kilo milioni 250 kwa mwaka 2020.

Sababu zinazopelekea kushuka kwa soko la Chai nchini humo ni pamoja na hatua ya serikali kupunguza matumizi ya zao hilo linalotumika kwa wingi, hali ambayo imepelekea kupungua kwa kilo milioni 2 za mauzo katika soko la ndani, hapo awali kilo miloni 20 ziliuzwa kwa soko la ndani na hivi sasa ni kilo milioni 18 pekee huuzwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live