Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umoja wa Ulaya kujadili Rwanda kuondolewa vikwazo vya usafiri

B21159d41990ccaf28c1a100c83a60e9 Umoja wa Ulaya kujadili Rwanda kuondolewa vikwazo vya usafiri

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BARAZA la Umoja wa Ulaya (EU) limeiorodhesha Rwanda kati ya nchi zinazopaswa kuondolewa vizuizi vya kusafiri kwenda katika nchi hizo.

Hatua hiyo ilipitishwa chini ya pendekezo juu ya kuondolewa polepole kwa vizuizi vya safari kwenda Umoja wa Ulaya.

"Kuanzia Septemba 23, nchi wanachama zinapaswa kuondoa polepole vizuizi vya kusafiri katika mipaka ya nje kwa wakazi wa nchi zifuatazo," ilisomeka taarifa hiyo kutoka kwa baraza wakati inataja Rwanda.

Orodha hiyo pia inajumuisha nchi zinazoondolewa vikwazo kuwa ni Chile, Kuwait, Singapore, Canada, Australia, Jordan, New Zealand na Ukraine na nyingine.

Kuondoa vizuizi vya kusafiri, EU inazingatia vigezo tofauti pamoja na hali ya ugonjwa, utoaji wa majibu ya jumla ya ugonjwa wa Covid-19, na pia kuaminika kwa habari na vyanzo vya takwimu.

Marufuku ya kusafiri imeondolewa kutoka Rwanda, baada ya nchi hii kupongezwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kwa kufikia lengo lililowekwa kufikia Septemba 2021, la kutoa chanjo kwa asilimia 10 ya idadi ya watu.

Wakati takwimu za maambukizi ya Covid-19 zimeshuka, nchi hii imeondoa vizuizi kadhaa vya Covid-19 vikiwemo vya kutotoka nje zilivyosogezwa hadi saa 11:00 jioni wakati shule na sehemu za ibada zikifunguliwa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz