Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulimwengu auwasha Mazembe

Ulimwengu Pic Data Ulimwengu auwasha Mazembe

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

STRAIKA Mtanzania Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe huu umeonekana kuwa mwaka wake baada ya kuwa sehemu ya mafanikio katika kikosi hicho kwa kuifungia mabao muhimu timu hiyo.

Ulimwengu amekuwa na msimu bora licha ya kuanza kwa kusuasua lakini mpaka sasa ameifungia timu hiyo mabao nane katika mechi 16 kwenye Ligi Kuu nchini humo na matatu Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumzia kiwango chake, Ulimwengu alisema jambo kubwa linalomfanya apambane ni kuhakikisha timu yake ichukue ubingwa wa ligi msimu huu.

“Nashukuru kwanza kurejea katika kiwango changu, hili ni jambo zuri kwangu na malengo yangu msimu huu ni kuhakikisha timu inachukua ubingwa.

Kila kitu kinawezekana katika ufungaji bora ukiweka nia, tuna mechi nne na nipo nafasi ya tatu kwenye wafungaji natamani niwe naongoza au nishike nafasi ya pili.” alisema Ulimwengu

Mshambuliaji huyo alipitia wakati mgumu baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu, msimu uliopita alirejea Mazembe.

Mazembe kwenye ligi ya nchi hiyo inaongoza ikiwa na pointi 63, wa pili As Vita wakiwa na pointi 61.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz