Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujuzi wakwamisha uzalishaji Afrika Mashariki kwa 77%

SKILL GAPE Ujuzi wakwamisha uzalishaji Afrika Mashariki kwa 77%

Thu, 14 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Suala la ukosefu wa ujuzikatika maeneo ya kazi limetajwa kuathiri uzalishaji kwa asilimia 77, ufanisi kwa asilimia 42 na ushindani kwa asilimia 8 katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa takwimu zilizofanyika hivi karibuni ambazo zinaonesha asilimia 65 ya Wakurugenzi Watendaji barani Afrika wanaamini kuwa ukosefu wa ujuzi unazuia mashirika, viwanda, kampuni na Taasisi kuweza kufikia malengo waliojiwekea.

Haya yameibuliwa katika mkutano wa pamoja wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki EABC na Nelson Mandela African Institution of Science NM-AIST na kujadili kuhusu njia za kuiba pengo hilo.

Aidha wamekubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili kuweza kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia katika Umoja wa Nchi za Afrika Mashariki EAC.

Takwimu hizi ni kwa mujibu wa kituo cha viwango cha Afrika Mashariki EAOFHE, na katika tafti zilizofanyika mwaka 2014 zinaonesha athari za pengo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live