Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi wa 'Kigali Green City' wasogweza mpaka 2023

Rwanda Delayed Ujenzi wa 'Kigali Green City' kumalizika 2023

Fri, 24 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makadirio ya kumalizika kwa ujenzi wa nyumba za kisasa katika jiji la kigali uliopewa jina la 'Kigali Green City' wilayani Gasabo yamesogezwa mbele hadi mwaka 2023 kufuatia kusuasua kwa utekelezaji wa mradi huo.

Ujenzi huo ambao ni wa mapinduzi ya kijani ulitazamiwa kuanza mwezi Januari mwaka 2020 katika eneo lenye hekari 620 kwa matazamio ya kukamilika mwezi Disemba mwaka 2020.

Ucheleweshwaji wa mradi huo umesababishwa na mazingira mabovu ya kufanyia kazi pamoja na uhaba wa vitendea kazi katika muda husika.

Nayo taasisi inayofadhili mradi huo ya 'Rwanda Green fund' imesema kuwa imenuia kuboresha mradi huo kwa kuongeza fedha za kuratibu kutoka dola bilioni 4 sawa na trilioni 9.27 za kitanzania, hadi dola 5 sawa na trilioni 11.59 za Tanzania.

Mradi huo umelenga kujenga makazi 30,000 yatakayochukua watu zaiidi ya 150,000 huku ukitazamiwa kutengeneza ajira kwa watu 16,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live