Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yatinga fainali Afcon U20

Uganda Pic Data Uganda yatinga fainali Afcon U20

Tue, 2 Mar 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Eliya SolomonMore by this Author TIMU ya taifa ya Uganda kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20, imetinga fainali ya Afcon U20 huko Mauritania baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Tunisia.

Wababe hao kutoka ukanda wa Afrika Mashariki ni miongoni mwa timu nne ambazo zimejikatia tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia kwa vijana wenzao wenye umri chini ya miaka 20 ambazo hata hivyo ziliahirishwa kutokana na janga la virusi vya corona.

Aliyekuwa mwiba mkali kwa Watunisia katika mchezo huo wa  nusu fainali alikuwa ni Derrick Kakooza ambaye alitupia mabao matatu 'hat trick' dakika ya 37, 50 na 73.   

Uganda walionekana kutandaza soka safi na kuwazidi mbinu wapinzani wao ambao walionekana kushindwa kufua dafu na kujikuta wakikumbana na kipigo cha mabao 4-1, bao la kufutia machozi kwa Tunisia lilifungwa na Ben Lamin dakika ya 39.

Aliyefungua akaunti ya mabao kwenye mchezo huo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Olympique  mjini Nouakchott, Mauritania  alikuwa Richard Basangwa dakika ya nne tu.

Fainali ya mashindano hayo inatarajiwa kuchezwa Jumamosi, Machi 6 na Uganda watakuwa na kibarua kizito cha kucheza dhidi ya vijana wenzao wa Ghana ambao kwenye mchezo wa kwanza tu katika hatua ya makundi waliinyuka Tanzania mabao 4-0.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz