Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda yapata wasambazaji vifaa EACOP

EACOPTZUG Uganda yapata wasambazaji vifaa EACOP

Tue, 5 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tayari Uganda imeanza kupanga safu ya wasambazaji wa vifaa vya ujenzi wa bomba la mafuta nchini Tanzania EACOP kabla ya kuanza rasmi kwa ujenzi huo mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Nae Meneja Mkuu wa EACOP , Martin Tiffen amefafanua maendeleo ya ujenzi huo wakati wa Mkutano wa siku mbili wa Mafuta na Gesi wa Uganda UIOGS, na kusema kuwa mikataba ya wasambazaji hao itasainiwa pindi taratibu za kisheria na kibiashara zitakapo kamilika.

"Tayari tumeshakamilisha mchakato wa kuwapata Wakandarasi wanne muhimu waliokidhi vigezo tulivyoviweka" amesema Meneja huyo.

Amebainisha kuwa EACOP ina idadi kubwa ya wasambazaji wa vifaa vya ujenzi huo na tayari wamejipanga kukutana nao ili kuweza kufikia makubaliano ya usambazaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live