Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda kuuza maziwa Zambia, Mzozo wa Kenya watajwa

Maziwa Data Uganda kuuza maziwa Zambia, Mzozo wa Kenya watajwa

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Uganda imefanikisha kutatua kitendawili cha soko la maziwa kilichokuwa kimebaki bila majibu mara baada ya Kenya kusitisha uingizwaji wa bidhaa hiyo mwezi Disemba 27, 2021.

Haya yamebainishwa na Waziri wa kilimo nchini humo, Frank Tumwebaze na kueleza kuwa wameingia makubaliano na Zambia na kuwa kuanzia sasa watakuwa wakisafirisha bidhaa hiyo nchini humo.

Waziri huyo amefanikisha kusafirisha jumla ya tani 50 za maziwa ya unga kwenda katika kiwanda cha Coca Cola cha Zambia, hatua ambayo aliita kuwa ya kicheko kwa wazalishaji wa bidhaa hiyo nchini humo.

Hata hivyo kiwanda hicho kitakuwa kikiagiza jumla ya tani 700 za maziwa kwa mwaka.

Kenya ndiyo ilikuwa kitovu kikuu cha usafirishaji wa bidhaa hiyo kabla ya kusitishwa na mamlaka za nchini humo, jitihada kadhaa zimeshafanywa ambazo hazijazaa matunda huku kukishuhudiwa kuwepo kwa ongezo kubwa la ushuru wa usafirishaji pindi bidhaa hii inapofikishwa nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live