Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda kuingiza trilioni 9.22 maonesho ya Dubai

Uganda  Expo Uganda kujipatia trilioni 9.22 maonesho ya Dubai

Fri, 8 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uganda inatarajia kushiriki maonesho ya biashara yanayoendelea Dubai yatakayo chochea uwekezaji wenye thamani ya dola bilioni 4 sawa na trilioni 9.22 za kitanzania kwenye sekta tofauti tofauti nchini humo kufika mwaka 2022.

Maonesho hayo yaliyoanza Oktoba 1, 2021 yamezivutia nchi takribani 200 pamoja na wawekazaji nguli duniani.

Taarifa hii ya ushiriki imetafasiriwa na mamlaka za Uganda kama ishara kubwa ya uwekezaji nchini humo.

" Taarifa hii ya uwekezaji ni sehemu ya mipango ya Serikali na tutahakikisha kuwa tunafanya uwekezaji wa dola bilioni 4 ili kuweza kuipandisha nchi yetu mbele kiuchumi hasa katika kipindi hiki ambacho tumeathirika na janaga la Corona" amesema Roberty Mukiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Uganda.

Mkurugenzi huyo ameongeza kusema kuwa Serikali inatazamia kufanya uwekezaji mkubwa katika miradi ya maendeleo 79 katika maeneo tofauti nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live