Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda kufanya mazungumzo na Kenya mzozo soko la Maziwa

Mlikyexpog Uganda kufanya mazungumzo na Kenya mzozo soko la Maziwa

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uganda imealika timu ya Kilimo na biashara kutoka Kenya kwenda Kampala kwa ajili ya kufanya mazungumzo ili kuondoa vikwazo vya kibiashara vilivyopo kwenye uagizaji wa bidhaa ya maziwa yanayozalishwa Uganda.

Miezi miwili iliyopita Kenya iliongeza ushuru wa asilimia 7 kwenye bidhaa hiyo, jambo amblo limeonekana kwenda kinyume na makubaliano ya Umoja wa nchi za Afrika Mashariki.

Kamishna Mkuu wa Uganda nchini Kenya Dk.Hassan Wasswa Galiwang, amesema kuwa Uganda tayari imeshatuma mwaliko kwa timu hizo kwa ajili ya kutatua suala hilo ili kuruhusu nchi zote mbili kunufaika kibiashara.

"Uganda ilitakiwa iwe inaingiza bidhaa hii hapa Kenya, lakini kuna chanagamoto kadhaa ambazo zitatuliwa siku si nyingi, tayari tumeshatuma mwaliko kwa Serikali ya Kenya ambao watafanya ukaguzi kwenye viwanda vinavyozalisha bidhaa hii, ili kujihakikishia soko la bidhaa hii" amesema Kamishna huyo.

Mzozo huu ulianza tangu mwezi Julai 2021, wakati Waziri wa Kilimo nchini Uganda, Frank Tumwebaze alipotoa ombi kwa Kenya na Tanzania kuruhusu bidhaa hiyo iingizwe katika masoko ya nchi hizo mbili, mpango ambao haukufanikiwa kutokana na changamoto za janga la Corona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live