Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda imeuza Bangi ya Tsh. Bilioni 4.4 kwenda Ujerumani

CANNABISS MEDI Uganda imeuza Bangi ya Tsh. Bilioni 4.4 kwenda Ujerumani

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Uganda imefanikisha kusafirisha Kilo 400 za Bangi maalumu inayokwenda kutumika kwa aajili ya dawa nchini Ujerumani. Hii inakua ni shehena ya nne kutoka Uganda kwenda nchi nza nje tangu nchi hiyo iliporuhusu kilimo cha Bangi.

Imeelezwa kuwa kilo moja ya Bangi ya Dawa (MC), ambayo inatajwa kutumika kama tiba ya magojnjwa mengi ikiwemo Saratani, inagharimu Euro 4,300 ambayo ni zaidi ya Tsh. Milioni 11 za Tanzania. Na hii ni kwa mujibu wa mtandao wa www.gmp-compliance.org unaendeshwa na taasisi ya nchini Ujerumani ambayo inahusika na tafiti za makampuni yanayozalisha bidhaa za matibabu na afya.

Mr Benjamin Cadet, ni mmoja kati ya Wakurugenzi wa Industrial Hemp Uganda Ltd, kiwanda kilichopewa leseni ya serikali ili kufanya kilimo cha Bangi ya Dawa amesema kuwa wamefanikiwa kusafirisha kiasi hicho cha Bangi wiki iliyopita October 16.

Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani 30 kwa mwaka lakini kutokana na janga la Corona uzalishaji umekua hafifu tofauti na matarajio yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live