Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda hoi Afcon ya ufukweni

75a05fb8516e3eaa7337a7f3f1d024d9.jpeg Uganda hoi Afcon ya ufukweni

Tue, 25 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU ya taifa ya Uganda (Uganda Sand Cranes) ya soka la ufukweni imeanza vibaya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Soka la Ufukweni (Afcon) baada ya kupokea kichapo cha mabao 5-1 kutoka kwa wenyeji Senegal.

Katika mchezo huo wa Kundi A, Uganda walijikuta wakianza vibaya mashindano hayo ambayo wanashiriki kwa mara ya kwanza fainali hizo.

Wenyeji Senegal walipata bao la kuongoza na mengine mawili ndani ya dakika 20.

Mabao ya timu hiyo kutoka Afrika Magharibi yalipatikana kupitia kwa Royal Mendy na Fah Babacas ambao kila mmoja alifunga mawili n jingine lilipatikana kupitia kwa Ninou Diatta.

Timu hiyo haitakuwa na muda wa kupumzika, kwani jana ilitarajiwa kucheza dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Tanzania.

Kocha Msadizi wa Uganda, Bashir Mutyaba amesema Senegal ni timu yenye uzoefu mkubwa na soka hilo la ufukweni ikilinganishwa na wao, lakini wamejifunza mengi kutoka kwao.

“Tunajifunza kutokana na makosa ili kuhakikisha tunafuzu kwa raundi nyingine. Senegal ni moja ya timu imara sana na yenye uzoefu mkubwa na imeshinda taji hilo mara saba na imeshacheza Kombe la Dunia la soka la ufukweni,” alisema Mutyaba.

Wakati huohuo, Msumbiji iliifunga Misri kwa mabao 7-5 na Morocco iliichakaza Shelisheli kwa mabao 5-1 katika mechi zingine mbili zilizochezwa juzi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz