Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchumi wa dunia kushuka zaidi ya 6%- IMF

Aslmia 66 Uchumi wa dunia kushuka zaidi ya 6%- IMF

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Fedha la Kimataifa kupitia kwa kiongozi wake Mkuu, Kristalina Georgieva limesema kuwa uchumi wa dunia unatarajiwa kushuka zaidi ya asilimia 6 zilizokadiliwa kushuka kwa mwezi Julai mwaka 2021.

Shirika hilo limetaja sababu za kushuka kwa uchumi kuwa kukithiri kwa madeni kutoka katika mataifa mengi duniani, mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa, kubadilika kwa mwenendo wa uchumi, pamoja na janga la Corona linaloendelea kusumbua dunia yote kwa sasa.

Georgieva amesema kuwa janga la Corona limekuwa kikwazo kikubwa katika kupanda kwa uchumi wa dunia na kuongeza kuwa licha ya kupatikana kwa chanjo ya ugongwa huu bado ahueni ya kiuchumi haijafikiwa.

"Bado hatujapata mwarobaini wa kushuka kwa uchumi, ugonjwa huu wa Corona ni tishio katika ustawi wa uchumi, athari zake ni kubwa na zinaondoa matumaini" amesema kiongozi huyo.

Aidha ametoa tahadhari ya mfumuko wa bei za bidhaa kwa kusema kuwa kama hali itaendelea hivi basi uchumi wa mataifa yanayoendelea utaathirika zaidi, pia ameitaja Marekani na China kuwa moja ya mataifa yaliyojitahidi kudhibiti mtikisiko huu wa kiuchumi.

Hata hivyo amebainisha kuwa ahueni ya kiuchumi inatarajiwa kufikiwa mnano mwaka 2022 huku mataifa baadhi yanayoendelea kiuchumi yatakuwa yakikiabiliwa na athari kiasi za kiuchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live