Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchumi wa Burundi kupanda kwa asilimia 4.3 mwaka huu

Burundi Country Portal Uchumi wa Burundi kupanda kwa asilimia 4.3 mwaka huu

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la fedha Duniani IMF limesema kuwa Uchumi wa Burundi unatarajiwa kupanda kwa asilimia 4.3 mwaka huu wa 2024 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Katika ripoti IMF inasema kuwa uchumi huo unatarajiwa kupanda kupitia sekta ya kilimo hasa zao la Kahawa.

IMF imebainisha kuwa ukosefu wa mafuta nchini Burundi kwa mwaka uliopita ni miongoni mwa chanzo cha uchumi wa Burundi kushuka kufikia asilimia 2.7 na kuwa nchi ya kwanza kwa umaskini Duniani.

Mwaka uliopita IMF iliidhinisha mkopo wa dola milioni 261.7 za Kimarekani kwa muda wa miezi 38 ambazo zitasaidia katika Nyanja mbali mbali ikiwemo kilimo na maendeleo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live