Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twitter kufunguliwa Nigeria endapo itafuata masharti ya serikali

Twitter And Buhari.jpeg Twitter kufunguliwa Nigeria endapo itafuata masharti ya serikali

Fri, 1 Oct 2021 Chanzo: BBC

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameamuru kuondolewa kwa marufuku dhidi ya mtandao wa kijamii wa Twitter, ikiwa tu kampuni hiyo ya kubwa ya teknolojia itafikia masharti flani.

Rais Buhari amesema Wanigeria wanaweza kuendelea kutumia mtandao huo kwa ajili ya "biashara na masuala mengine muhimu".

Katika hotuba yake ya kuadhimisha siku kuu ya uhuru wa nchi hiyo, Rais alisema kwamba kamati maalum ya ofisi yake inajadiliana naT witter kuhusu masuala kadhaa ya usalama wa kitaifa, ushuru wa haki na utatuzi wa mizozo.

Serikali ya Nigeria ilipiga marufuku huduma za Twitter tangu mwezi Juni baada ya mtandao huo wa kijamii kufuta ujumbe tata wa Rais Buhari.

Marufuku hiyo ilikosolowe vikali na mashirika ya kutetea haki za binadamu na wanaharakati wa kutetea uhuru wa vyombo vya habari.

Chanzo: BBC