Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

''Tutapambana hadi nukta ya mwisho'' - Giggs

BEACH SOCCER 0.jpeg ''Tutapambana hadi nukta ya mwisho'' - Giggs

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: eatv.tv

Nahodha wa timu ya Taifa ya Burundi kwa mchezo wa soka la ufukweni 'beach soccer' Ishimwe Giggs amejinasibu kuifunga timu ya Tanzania katika mchezo wa pili wa marudiano unaotizamiwa kuchezwa tarehe 3/04/2021 baaada ya ule wa kwanza uliochezwa Jumanne hii kumalizika kwa kufugwa 8-3.

Submitted by Tigana Lukinja on Alhamisi , 1st Apr , 2021 Mchezo wa kwanza wa Burundi vs Tanzania

''Kuna vitu vilitutatiza katika mchezo wa kwanza, ikiwemo kadi nyekundu tuliyoipata ilituchanganya sana na kutufanya kupoteza mbinu zetu za kiufundi kwa kuwa tulikuwa hatutimii, lakini kwa sasa tumefanyia marekebisho baadhi ya mambo na hakika tunakwenda kuwafunga Tanzania,'' alisema Giggs.

''Tanzania ni wepesi na wanafungika bila tatizo lolote, tumejua ubora wao upo wapi na udhaifu wao hali kadharika, hivyo basi tunaenda kupindua meza kila moja wetu fikra zake zipo kwenye kufuzu michuano hii,'' aliongeza nahodha huyo.

Katika mchezo wa kwanza Tanzania waliibuka na ushindi wa bao 8-3 ambapo Burundi ndiyo walikuwa mwenyeji wa mchezo huo licha ya michezo yote miwili kupangwa kuchezwa hapa nchini. Mshindi wa mechi hizi mbili atawakilisha AFCON mwezi wa 5 nchini Senegal.

Mchezo wa soka la ufukweni bado ni mgeni kwa ukanda huu wa Africa Mashariki. Burundi wao walianza kucheza mwaka 2006 na Tanzania walianza kucheza 2014

Chanzo: eatv.tv