Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tume ya Mawaziri Kenya kuchunguza bei ya umeme

Kenya Powers Tume ya Mawaziri Kenya kuchunguza bei ya umeme

Fri, 8 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tayari tume ya mawaziri imeundwa nchini Kenya ili kufanya ukaguzi wa usambazaji wa umeme, uhitaji wa huduma hiyo, sera pamoja na bei elekezi zilizowekwa na shirika la umeme la Kenya Power.

Hatua hii imekuja siku kadhaa baada ya Rais Kenyatta kutangaza punguzo la asilimia 33 kwenye manunuzi ya umeme litakalo anza kutumika mwezi Disemba 2021.

Nae Katibu wa Uratibu wa Mambo ya ndani ya Serikali nchini humo Fred Matiang'i amesema kuwa Kenya Power imetangaza mradi maalumu utakaowezesha upatikanaji umeme nchi nzima, na kuongeza kuwa tume hiyo itasimamia mageuzi ya kiutendaji katika Shirika hilo.

"Tutafanya ukaguzi kwenye mifumo inayotumika kuendesha kampuni yetu ya umeme ya Kenya Power, tuna shirikiana kwa pamoja na tume hii ya mawaziri ili kudhibiti uharibifu mkubwa uliofanyika katika shirika hili, tutashughulikia changamoto zote zinazo sababisha kupanda kwa gharama za manunuzi ya umeme" Amesema Katibu huyo.

Amezitaja sekta nyingine zitakazo shirikiana na Tume hiyo kuwa ni pamoja na Bodi ya Upelelezi wa makosa ya Jinai, Kituo cha ripoti za fedha cha Benki Kuu pamoja na Wakala wa urejeshi wa Mali nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live