Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Toyota yatangaza kutengeneza magari ya umeme yatakayotajirisha Afrika

Toyota Afrika Uzalishaji magari ya umeme kuitajirisha Afrika

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya kutengeneza magari ya Toyota imetangaza kufanya uwekezaji mkubwa katika kutengeneza magari pamoja na vifaa vyake vya umeme, hatua ambayo imepokelewa kwa shangwe na nchi zenye utajiri wa madini barani Afrika.

Hatua hii ya Toyota inakuja wakati ambapo kampuni nyingi za uzalishaji wa Magari zikiwa katika mchakato wa kutoka katika kutengeneza magari yanayotumia mafuta kwenda kwenye umeme, jambo ambalo linakadiriwa kuja kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa miaka ijayo ikiwa ni pamoja na kwa kuziongezea nchi nyingi za barani Afrika mabilioni ya fedha.

Aidha uzalishaji wa Magari hayo unategemea kwa kiasi kikubwa madini ya nickel, aluminium pamoja na chuma, ambayo yanapatika kwa wingi barani Afrika, hali hii inatajwa na wachambuzi wa uchumi kuwa itaongeza uhitaji mkubwa wa madini haya hivyo kuziongezea pato nchi zinazozalisha madini hayo. Kampuni hiyi imetangaza mpango huo na kusemakuwa itawekeza kiasi cha dola bilioni 13.6 sawa na Shilingi za kitanzania trilioni 30.14

Chanzo: www.tanzaniaweb.live