Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania na Kenya zaongoza kwa ubunifu Kusini mwa Afrika

Kenya Tanzaniaee Tanzania na Kenya zaongoza kwa ubunifu Ukanda wa Kusini mwa Afrika

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Utafiti uliofanywa na Shirika la Global Innovation Index la Afrika Kusini, umeoesha kuwa Tanzania na Kenya zimeshikilia nafasi ya tatu katika masuala ya ubunifu katika nchi za ukanda wa Kusini mwa Afrika.

Hata hivyo taifa la Kenya limekamata nafasi ya 85 kidunia huku Tanzania ikiwa nafasi ya 90 katika orodha ya nchi bora 100 kwa ubunifu, hali hii imezifanya nchini hizi kuongoza katika ukanda huu.

Orodha hii hutolewa kila mwaka na Shirika la Hati Miliki Ulimwenguni (WIPO), ambapo ubunifu huu unatazamwa katika ustawi wa sekta mbali mbali katika kila taifa, zinazochochea kuboresha maisha ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuleta maendeleo.

Aidha hatua hii inatajwa kuchangiwa na usuluhishi wa vikwazo vya kibiashara uliofikiwa na Marais wa nchi hizi mbili kwa kuondoa mlundikano wa kodi uliokuwepo hapo awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live