Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanasha Anukia Wasafi

TANASHA 6.png?fit=1280%2C720&ssl=1 Tanasha Anukia Wasafi

Tue, 11 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Tanasha Anukia Wasafi May 11, 2021 by Global Publishers



MWANAMAMA kutoka nchi jirani ya Kenya, Tanasha Donna Oketch amesikika vizuri kunako muziki wa kizazi kipya.

Katika miaka yake miwili kwenye muziki, ameweka rekodi mbalimbali. Jina la Tanasha lilikua kubwa baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na megastaa wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Katika mapenzi yao, wawili hao walijaaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Naseeb Junior kabla ya kutengana mwanzoni mwa mwaka jana.Kwenye sanaa, Tanasha alianza kama miss akishiriki mashindano mbalimbali, kabla ya kujikita kwenye mitindo na ubunifu wa mavazi.

Kwa mara ya kwanza alianza kuuza nyago kama video vixen (video queen) kwenye ile Ngoma ya Nagharamia ya mtu mzima, Christian Bella aliyomshirikisha King wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.

Baada ya kujikita kwenye muziki yapata miaka miwili sasa, Tanasha amekiwasha mno na ngoma mbalimbali zilizokamata chati kibwena za muziki kwa Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla.Hata kama mwenyewe hajasema, lakini shukrani nyingi ziende kwa Diamond aliyemtambulisha kwenye ulimwengu wa ustaa kupitia muziki kwa ile ngoma yao ya pamoja ya Gere.



Mbali na Gere ambayo ilifanya vizuri na inazidi kufanya vizuri kwenye platforms mbalimbali za kusikiliza, kutazama, kuuza na kununua muziki, Tanasha amesikika na ngoma nyingine kali kama, La Vie akiwa na Mbosso Khan, Sawa, Te amo, Ride, Na Wewe, Kalypso na nyinginezo.

Sasa, taarifa nzito za ndani zinasema kwamba, Tanasha yupo njiani kumfuata Zuchu ambaye ni mwanamke wa mwsiho kusainiwa kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya Diamond.

Inavyoonekana, muziki wa Tanasha umeanza kutambulika nyumbani na nje ya nyumbani kwao hivyo anatafuta jukwaa la ‘kujiuza’ zaidi kimataifa na wengi wanamshauri afanye juu ya chini ili atue Wasafi.Kinachoonekana, kuna kampeni zimeendelea za kumuingiza Tanasha ndani ya Wasafi kufuatia nguvu inayotumiwa na Makamu wa Rais wa Wasafi, Romeo Jones ‘Rommy Jones’.Rommy anadai kwamba, amekuwa akifuatilia kwa karibu muziki wa Tanasha ana anaona wazi umekua.



Kumbuka; Rommy anatajwa kuwa ni injini kwenye muziki wa Wasafi na anaingia kwenye vikao vya juu kabisa vya uamuziki vya menejimenti na ana kura ya muhimu (veto) katika kuamua msanii anayestahili kusajiliwa Wasafi.Taarifa za ndani zinasema kwamba, ni miongoni mwa watu waliokuwa wakimfuatilia Zuchu kwa takriban miaka minne kabla ya kusema anastahili kusainiwa Wasafi.

Maoni ya Rommy yanakuja muda mfupi baada ya Tanasha kuposti msururu wa picha zake ‘tamu’ kwenye ukurasa wake wa InstagramKwenye picha hizo ndipo Rommy anajitokeza na kusema kuwa, mwanamama huyo yupo kwenye projekti yake mpya ya muziki; ikiwa ni wiki kadhaa tu zimepita tangu alipoachia wimbo mwingine mpya.

Alichokifanya Rommy inaaminika kulikuwa na mawasiliano kati yake na Tanasha hivyo maoni yake ikawa ni sehemu ya kumtia moyo kuendelea kufanya muziki mzuri ili kufanikisha ndoto yake ambayo hakuitaja.“Tanasha Jorja Smith Donna…” aliandika Rommy kwenye picha nyingine.

Maoni ya Rommy yanaonesha kuwa kuna kila dalili za Tanasha kunukia pale Wasafi kwani kwa sasa inasemekana kuwa memba wengi wa jamii ya Wasafi wanamkubali bila kusahau ana mtoto wao, Naseeb Junior.

Kwanza kabisa, Tanasha anabebwa na Diamond ambaye amezaa naye hivyo siyo rahisi kupigwa kujiunga na lebo hiyo ambayo baba mtoto wake huyo ndiye C.E.O wake.

Pia kuna taarifa za ndani kwamba, anaweza akasainiwa, lakini akabaki kwenye tawi la Wasafi linalofunguliwa Nairobi nchini Kenya muda siyo mrefu.

Pili; Tanasha amekuwa akionesha kuvutiwa mno kufanya kazi za sanaa nchini Tanzania na amekuwa akifuatilia kwa ukaribu mambo ya Tanzania.Pamoja na kwamba Rommy anaonesha kuvutiwa kufanya kazi na Tanasha, lakini haina maana itakuwa ni haraka mno hata kama yeye ni makamu wa rais na ana cheo kikubwa kwenye lebo hiyo.

Kama uongozi, Wasafi hawajawahi kusema chochote juu ya kumsaini Tanasha, lakini yeye mwenyewe amewahi kusema haya; “Nadhani aina ya muziki ambayo ninafanya ukilinganisha na Wasafi ni tofauti kabisa, labda waanzishe Wasafi Caribian au Wasafi Hip Hop au kitu kama hicho labda.

”Tanasha anasema mpenzi wake, Diamond na timu nzima ya Wasafi wamekuwa wakimsapoti, lakini haoni nafasi yake ndani ya timu hiyo kutokana na aina tofauti ya muziki anayofanya

Chanzo: globalpublishers.co.tz