Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takriban watu 600 wauawa katika mapigano Sudan

UN Yatoa Wito Wa Kusitishwa Kwa Mapigano Wakati Wa Ramadhani Huko Sudan Takriban watu 600 wauawa katika mapigano El Fasher Sudan

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 600 wameuawa tangu Mei 10 katika mapigano yanayoendelea kati ya Wanajeshi wa Sudan (SAF) na Wanajeshi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko El Fasher, makao makuuu ya Jimbo la Darfur ya Kaskazini.

Ibrahim Khatir, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya ya Jimbo la Darfur Kaskazini ametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa rekodi rasmi, watu wasiopungua 600 wameuawa na takriban 4,500 wamejeruhiwa huko El Fasher tangu Mei 10 mwaka huu.

Amesisitiza kuwa, idadi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi kwani baadhi ya wahanga walizikwa moja kwa moja na familia zao bila kutoa taarifa hospitalini.

Vile vile ameitaja hali ya kiafya katika mji wa El Fasher kuwa ni "tulivu kiasi," licha ya hospitali nyingi na vituo vya afya katika jiji hilo kufungwa kutokana na mashambulizi ya mizinga.

Sudan imekumbwa na mzozo mbaya wa uchu wa madaraka katika ya majenerali wa kijeshi wanaoongoza pande mbili hasimu za SAF na RSF tangu Aprili 15, 2023 na kusababisha vifo vya watu 16,650. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya mwezi Juni ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu.

Takwimu zilizochapishwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa mwezi Juni zilionyesha kuwa zaidi ya watu milioni 7.7 walikuwa wameshakimbia makazi yao ndani ya Sudan tangu mgogoro huo uanze, huku takriban wengine milioni 2.2 wakitafuta hifadhi katika nchi jirani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live