Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars yaifuata Harambee Stars

1172a53f2c24a939e0dac276f1c91af3 Taifa Stars yaifuata Harambee Stars

Mon, 15 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliondoka jana kwenda Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kucheza michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo, ‘Harambee Stars’.

Taifa Stars ambayo iliingia kambini Machi 8 na kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam chini ya kocha Kim Poulsen imeondoka huku kocha akisema atatumia michezo hiyo kujua udhaifu wa timu.

Akizungumza baada ya kuondoka, Kim Poulsen alisema kwenye mchezo huo wa kesho na ule wa Machi 18 atazingatia zaidi kwenye mbinu za kushambulia na kujilinda ili kuweka uwiano sahihi kuelekea mechi za kufuzu.

“Tunaondoka na wachezaji wote 23 kwa sababu nategemea kuwatumia kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Kenya utakayochezwa kesho kutwa (kesho) na kundi la wachezaji wengine watacheza mchezo wa Machi 18,” alisema Kim.

Alisema wachezaji wa timu ya Simba na wengine ambao hawajaripoti kambini watakuja moja kwa moja Kenya kuungana na timu kwa ajili ya mechi zitakazofuata.

Taifa Stars itaitumia michezo hiyo kwa ajili ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea utakaochezwa ugenini Machi 25 na dhidi ya Libya, Machi 30 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Taifa Stars ipo Kundi J ikiwa na pointi nne Tunisia wanaongoza wakiwa na pointi 10, Equatorial Guinea wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi sita na Libya wanashika mkia wakiwa na pointi tatu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz