Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sven sare zamuandama Morocco

Sven Pic 2 Data Sven sare zamuandama Morocco

Sun, 4 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

ALIYEKUWA kocha wa Simba SC, Sven Vandenbroeck anayeifundisha kwa sasa FAR Rabat yenye maskani yake Rabat, Morocco, ameandamwa na matokeo ya sare katika mechi za Ligi Kuu nchini humo maarufu kama Batola Pro.

Sven aliyeondoka Tanzania, Januari mwaka huu baada ya kuiongoza Simba kutinga makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ameiongoza FAR Rabat katika michezo mitano ya Batola Pro na kuifanya timu hiyo kuwa nafasi ya nne nyuma ya Olympic Safi.

Chini ya Mbelgiji huyo, FAR imeshinda michezo miwili dhidi ya RSB Berkane na Mouloudia Oujda na aina ya ushindi ambao wameupata kwenye michezo yote hiyo ni wa mabao mawili huku sare zikiwa tatu.

Kocha huyo, aliikuta timu ikiwa imepoteza michezo miwili na ushindi na sare mara moja moja mmoja, hivyo alikuwa na kazi kubwa ya kuleta mabadiliko kwenye kikosi hicho ambayo taratibu yameanza kuonekana kiasi cha kusogea hadi nafasi ya nne licha ya kwamba mwendo wao ni wa kinyonga kutokana na sare ambazo zinawaandama.

Akimuongelea kocha huyo, mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva anayeichezea Wydad Casablanca pia ya nchini humo alisema, Sven ni kocha mzuri anayefaa apewa muda wa kutosha ili kuitengeneza timu hiyo.

” Hajapoteza mchezo hata mmoja kwenye Ligi na matokeo ya sare sio mbaya sana kwake, kutokana na ugeni wake kwenye Ligi,”

Related Gomes: Manula haondoki Simba Lwanga awapa somo viungo“Bado sijakutana naye nadhani mbeleni tutakutana kwenye michezo ya Ligi. Kuhusu FAR Rabat ni miongoni mwa timu ngumu ambazo zimekuwa zikitoa ushindani kwenye Ligi na naamini kwa uwezo wake anaweza kuifanya kuwa bora zaidi,” alisema Msuva.

Timu ya Msuva, Wydad Casablanca ndio vinara wa Batola Pro, wanaongoza msimamo huo wakiwa na pointi 22 huku wakifuatiwa na mahasimu wao, Raja Casablanca wenye pointi 19, Olympic Safi wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 15 halafu timu ya Sven ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 13 sawa na Ittihad Tanger.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz