Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spika wa Bunge alala mahabusu

Spika Kaunti Kiambu Spika wa Bunge alala mahabusu

Fri, 22 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi, Benson Mutura amelazimika kulala mahabusu, baada ya kuhojiwa kwa takriban saa tano, katika makao makuu ya Idara ya Ujasusi wa Jinai (DCI) nchini Kenya.

Mutura ambaye anatuhumiwa kumuibia mwajiri wake, kwa kupitisha marupurupu ya usafiri, ilhali hakusafiri. Pia anakabiliwa na kosa la kutwaa kitambulisho cha afisa mmoja wa wa jeshi la polisi.

Spika huyo atakesha kwenye kituo cha polisi cha Muthaiga akisubiri kufikishwa mahakamani. Mutura aliandamana na wakili wake alipofika katika makao makuu ya DCI mwendo wa saa tano mchana na kuhojiwa kwa takriban saa tano.

Siku ya Jumatano Mutura alidai kwamba masaibu yake yalianza pale aliposema kwamba Mamlaka ya Kusimamia Jiji la Nairobi (NMS) ni taasisi haramu. "Kama ilivyo kwa sasa, NMs ni shirika lisilo halali kwani kuongezwa muda wake kuhudumu haukuzingatia kanuni na sheria," Mutura alibainisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: