Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba watanguliza mguu moja makundi CAF

81b75cab9c77067cae56506769a85c2e Simba watanguliza mguu moja makundi CAF

Sun, 17 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Wawakilishi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba wametanguliza mguu mmoja mbele kuelekea hatua ya makundi ya ligi hiyo mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa awali dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Katika mchezo huo, mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco dakika ya pili na Tadeo Lwanga dakika ya tano ya kipindi cha kwanza na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko Simba ikiwa mbele kwa idadi hiyo ya mabao.

Kipindi cha pili timu zote zilishambuliana kwa zamu, Galaxy wakijaribu kutafuta mabao ya kuzawazisha ila uimara wa mabeki wa Simba ulisadia kutoruhusu bao. Hivyo hivyo kwa Simba ambao walijaribu kutengeza nafasi ambazo hazikuzaa matunda.

Simba watasubiri mchezo wa pili utakaopigwa Oktoba 24, 2021 Uwanja wa Mkapa na endapo watashinda au sare yoyote basi itaendelea katika hatua ya makundi. Mabao yote yamefungwa na John Bocco.

Chanzo: www.habarileo.co.tz