Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika la ndenge Kenya laongoza kwa kutoza nauli ya juu zaidi Afrika

Kq Pic Data Shirika la ndenge Kenya laongoza kwa kutoza nauli ya juu zaidi Afrika

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la ndege la Kenya KQ, linatajwa kuuza tiketi zake kwa gharama ya juu zaidi kulinganisha na mashirika mengine ya ndege barani Afrika kama ya Ethiopia, Afrika Kusini na lile la Ufaransa.

Kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanywa na Jukwaa la ushindani Afrika ACP, inayozihusisha nchi 24 barani humu ulibaini kuwa KQ inatoza nauli ya juu kwa safari zote a ndani ya nchi na kimataifa kulinganisha na mashirika mengine ya ndege ya Afrika.

Pia utafiti huo umeonesha kuwa shirika hilo limepoteza soko kubwa kwa wapinzani wake wakuu wanaotoza nauli kwa gharama nafuu ambao ni Ehiopia Airlines, uganda Airlines pamoja na mashirika mengine mapya.

"Kenya Airways inatoza nauli ya juu kwa abiria kwa kila kilomita (APPK) kwa safari za ndani ya nchi, za kikanda, na zie za kimataifa" Imesema ripoti hiyo

Hata hivyo utafiti huo umeandika kuwa kwa baadhi ya safari KQ inatoza nauli kwa gharama nafuu kulinganisha na wapinzani wake ambazo pia zimetajwa kuwa ni safari chache sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live