Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika la ndege la Uganda laanza safari za Dubai

Dubai Entebbe Shirika la ndege la Uganda laanza safari za Dubai

Tue, 5 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Ndege la Uganda limefanya safari yake ya kwanza Dubai mara baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Shirika hilo kwa miaka miwili.

Nao maafisa wa Shirika hilo wamesema kuwa hatua hiyo itawasaidia wafanyabiashara kuweza kufanya shughuli zao kwa wepesi pamoja na wale wanaokwenda Dubai kwa ajili ya matembezi.

Wameongeza kusema hatua hii ina faida kubwa kwa taifa hilo kwani itakuza uchumi wa nchi na kukuza uhusiano baina wa kibiashara kwa mataifa hayo mawili.

"Umoja wa Falme za kiarabu hasa Dubai ni moja ya sehemu muhimu kibiashara, hivyo tumelenga kuboresha miundombinu itakayowavutia wafanyabiashara wote nchini" imesema taarifa ya Shirika hilo.

Hata hivyo Shirika hilo linaonelea kwa siku zijazo kufanya mkakati wa kuanzisha safari za Ulaya, Mashariki na Magharibi ya mbali kupitia Mikataba ya washirika wakubwa wa Dubai.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live