Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika la ndege la Kenya na Afrika Kusini zasaini Mkataba wa pamoja

SAA KQ Shirika la ndege la Kenya na Afrika Kusini zasaini Mkataba wa pamoja

Wed, 29 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Ndege la Kenya KQ na la Afrika Kusini SAA, zimeungana kwa pamoja ili kuinua mapato ya mashirika yote mawili yaliyoharibiwa na mlipuko wa ugonjwa Corona.

Wamesaini hati ya makubaliano yanayolenga kujenga na kukuza mashirika yote kwa pamoja ili kuweza kupambana na changamoto ambazo zinaikumba sekta ya usafiri wa anga duniani.

Nae Mtendaji Mkuu wa KQ, Allan Kilavuka amesema kuwa ushirikianao huo utasaidia kurejesha uchumi wa Mamlaka hizo uliotetereka kwa janga la Corona.

"Katika kujenga na kuboresha Mamlaka hizi za anga tumeona tufikie makubaliano haya ili kuweza kufikia malengo ya muda mrefu tuliojiwekea, na ushirikiano huu utasaidia kukuza ujuzi, utarahishisha usafirishaji wa mizigo,tutaboresha ugunduzi" amesema Mtendaji huyo.

Aidha Mtendaji Mkuu wa SAA, Thomas Kgokolo amesema kuwa ushirikiao huu unajumuisha mikakati ya kuinua uchumi wa mashirika yote mawili, pamoja na kubana matumizi, ameongeza kusema kuwamakubaliano haya yatawasaidia wafanyabiashara kuweza kusafirisha mizigo yao kwa gharama nafuu jambo ambalo litawasaidia kuweza kupata faida zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live