Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Ethiopia yaanza kuuza hisa za kituo kikuu cha mawasiliano

Ethio Telecom22 Serikali nchini Ethiopia kuuza hisa za kituo kikuu cha Mawasiliano kwa wawekezajibinafsi

Wed, 15 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya nchini Ethiopia, imetangaza kuzindua mchakato wa zabuni utakao wawezesha wawekezaji binafsi kununua hadi hisa 40 katika kituo kikuu cha mawasiliano ya taifa cha Ethio Telecom.

Wizara ya Fedha nchini humo , ambayo inaongoza mchakato wa zabuni, ilitoa ombi la pendekezo (RFP) la ubinafsishaji wa hisa hizo.

"Serikali imetoa ombi la pendekezo la ubinafisishaji wa hisa, ili kuiongezea thamani kampuni hii ya mawasiliano ya taifa, kwa kuongeza utendaji kazi, kuboresha miundo mbinu na kufanya mapinduzi kwenye teknolojia" imesema Wizara hiyo.

Aidha, taarifa ya Wizara hiyo imewataka wale wote walio na nia ya kutaka kuwekeza na kampuni hiyo kuchangamkia fursa mapema huku ikibainisha kuwa mchakato huo hauna vigezo vigumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live