Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya DR Congo imefuta zuio la wimbo unaomkosa Rais

Groupe Mpr Et Felix Tshisekedi 21 1 Jpg 640 350 1.jpeg Serikali ya DR Congo imefuta zuio la wimbo unaomkosa Rais

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: BBC

Maafisa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameondoa marufuku ya wimbo unaomkosoa Rais Félix Tshisekedi. Marufuku hiyo ilitangazwa Jumanne na tume ya udhibiti na kisha kuondolewa Jumatano baada ya waziri wa sheria kuingilia kati.

Kundi linalounga mkono muziki huo, MPR, pia lilisema limeomba marufuku hiyo kuondolewa. Marufuku hiyo ilikuwa imeonekana kuwa ya kidikteta na ilikosolewa sana.

Vyombo vya habari sasa vimeruhusiwa kupiga wimbo Nini Tosali Te (Nini Hatukufanya katika lugha ya Kilingala). Wimbo huo unalinganisha kile ambacho Bw Tshisekedi aliahidi alipokuwa kwenye upinzani na kile ambacho amefanikiwa kufikia sasa akiwa rais.

"Ulituahidi furaha baada ya [marehemu rais] Mobutu kuondoka. Mobutu alienda lakini hatukupata chochote. Ulisema ungerekebisha mambo ikiwa [rais wa zamani] Kabila atajiuzulu. Kabila aliondoka lakini bado ni ngumu," AFP. shirika la habari linanukuu maneno hayo yakisema.

Wimbo mwingine mmoja katika Kifaransa, Barua kwa Ya Tshitshi, jina la utani la marehemu babake Bw Tshisekedi, Etienne, bado umepigwa marufuku.

Mwimbaji, Bob Elvis, anasema: "Tangu uondoke, mwanao Felix amekuwa rais... Tumebadilisha utawala bila kubadilisha mfumo," AFP inaripoti.

Msemaji wa serikali Patrick Muyaya alitweet kwamba marufuku hiyo haikutoka kwa serikali.

“Mwananchi yeyote ana uhuru wa kutoa maoni yake, mradi yanazingatia sheria,” alisema.

Idadi ya kutazamwa kwa nyimbo hizo mbili imeongezeka kwenye YouTube tangu kupigwa marufuku, kulingana na tovuti ya habari ya Actualite Congo.

Chanzo: BBC