Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekta ya madini Uganda yatajwa kusuasua

Oil Uganda Sekta ya madini Uganda yatajwa kusuasua

Tue, 14 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya Serikali ya Uganda kufanya maboresho katika sekta ya Madini, mafuta na gesi, bado sekta hii inatajwa kuwa dhoofu kwa sababu ya utendaji legevu unaosababishwa na ubovu wa sheria zinazo ongoza sekta hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa na kituo cha Rasilimali cha taifa mwaka 2021, imeonesha kuwa sekta hiyo imepata alama 49 pekee licha ya Serikali kusajili sekta hiyo kwa alama 55 hali iliyopelekea upungufu wa alama 5.

Aidha kituo hicho kimetoa mapendekezo kwa Sekta ya madini nchini humo kuhakikisha wanaweka wazi taarifa za mapato na matumizi ili kuweza kupata matokeo bora katika sekta hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live