Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sarkodie abadili tarehe ya kuachia album,wiki hii kuachia ngoma mpya

5454545454333 629x400 Sarkodie abadili tarehe ya kuachia album,wiki hii kuachia ngoma mpya

Mon, 5 Jul 2021 Chanzo: millardayo.com

Ni Staa kutokea Nchini Ghana, Sarkodie ambae time hii ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kusitisha kuachia album yake aliyoipa jina la No Pressure ilitarajiwa kuachia tarehe 9 Julai, 2021, taarifa hiyo ameitoa kupitia ukurasa wake wa instagram na kuwaahidi ataiachia Julai 30, 2021.

Mbali na taarifa hiyo  amewaahidi mashabiki wake kuwa kuwa wiki hii  tarehe 9 ataachia mkwaju mpya.

Star wa hiphop kutokea nchini #Ghana @sarkodie amesitisha kuachia album yake #NoPressure iliyokuwa itoke julai, 9, 2021

Nyota huyu ametumia ukurasa wake wa instagram kuomba radhi kufuatia taarifa hiyo na kutoa tarehe rasmi ya kuachia album yake hiyo ambayo ni julai, 30, 2021

Hata hivyo katika taarifa yake hiyo #Sarkodie hakuwaacha hivi hivi mashabiki wake, kwani amewaahidi kuwapa ngoma mpya siku ya ijumaa hii tarehe 9

Chanzo: millardayo.com