Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sanaipei kazungumza kuhusu Maina Kageni walipokutana akiwa na miaka 21

2b51a8e485e634c0 Sanaipei kazungumza kuhusu Maina Kageni walipokutana akiwa na miaka 21

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mwimbaji wa Karaoke Sanaipei Tande anasema mtangazaji maarufu wa redio Maina Kageni alimtupia mistari alipojiunga na stesheni ya Kiss.

Sanaipei alisema alikuwa na miaka 21 wakati walikutana na Maina Kageni na mtangazaji huyo wa redio akaishiwa na nguvu. .

Alisema hakupoteza muda ila alimtaka awe kipusa wake kwa kumzalia mtoto lakini akasita kwa sababu alikuwa mchangaMaina alikuwa ameahidi kuhakikisha maisha yake yamelipiwa kila kitu ili asiwe akitafuta vibarua

Alisema umbo lake lilimmaliza Miana Kageni na hakusita kufungua moyo akimtaka awe mama wa mtoto wake.

Huwa ni wazi kwa wanamtandao kuwa Kageni humtamani sana Sanaipei na wenzake humtania kila wakati kuhusu hilo.

Sanaipei alisema alikuwa na umri wa miaka 21 na Maina alipomuona akamwambia amzalie mtoto na hilo litafungua njia zake kiuchumi.

Alifichua hayo alipokuwa katika mahojiano na mtangazaji Churchill kwenye kipindi chake cha kila Jumapili.

"Aliniambia hivyo nilipojiunga na Kiss 100FM na hata sikuwa nimepewa kipindi changu. Akaniambia kama sitaki kufanya kazi tena maishani mwangu nimzalie mtoto

Wakati huo bado nilikuwa mtoto, nilikuwa na miaka 21 na ndipo nilikuwa nikianza taaluma yangu naye Maina ananiambia kuhusu kuwa mama," alisema Sanaipei.

Alisema suala hilo la mvuto wake kwa Maina limekuwa moto hivi kwamba wanamtandao wanamtaja kila kuchao katika kuchangia mijadala ya Maina mtandaoni.

Wengi wanahisi kuwa anapoteza muda na nafasi bora kujijenga kwa kuendelea kudinda kuwa kipusa wa Maina.

Maina ambaye ni mtangazaji wa redio katika Classic FM anaaminika kuwa na mifuko mizito kutokana na umaarufu wake.

Kwenye taarifa nyingine, Sanaipei alisimulia jinsi alilazimika kuacha kuwa mwanamziki katika vilabu ili aweze kujiepusha na vileo.

Alisema kuenda kuimba katika vilabu ilikuwa ni chambo ya kumnasa na kumfanya kurudia maisha ya ulevi.

Anasema sasa amefaulu kuachana na vile na siku ya mwisho kuonja ilikuwa miaka miwili iliyopita.

Sanaipei hujulikana kwa sauti yake nyororo kama inayoskika kwenye wimbo wake maarufu wa Mfalme wa Mapenzi.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke