Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samuel Eto'o autaka Urais Shirikisho la Soka Cameroon

Etoo Samuel Fillis Samuel Eto'o

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa soka nchini Cameroon, Samuel Eto'o ametangaza nia yake ya kugombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini Cameroon. Tangazo hilo limetolewa Jumanne katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.

“Nimeamua kuchukua uamuzi huu kwa sababu ya kuipenda Cameroon na kupenda soka letu”, ameelezea Samuel Eto katika taarifa yake.

“Ni wakati wa kujenga upya mpira wetu”.

Baada ya uvumi kuenea, Eto'o ameamua kuweka hadharani nia yake ya kugombea nafasi ya juu katika mamlaka za Soka nchini Cameroon.

Ametangaza azma hiyo, huku ikiwa kuna utata juu ya marufuku ya uraia wa nchi mbili nchini Cameroon.

Samuel Eto alikuwa raia wa Uhispania wakati alipokuwa akichezea Hispania. Wakati miongoni mwa masharti yanayotakiwa kuwa mgombea wa urais wa shirikisho la mpira wa miguu la Cameroon, ni marufuku ya kuwa na utaifa wa kigeni.

Hata hivyo, bado haijulikani ikiwa ugombea wake utathibitishwa na mamlaka zinazosimamia uchaguzi huo. Uchaguzi umepangwa kufanyika Desemba 11.



Chanzo: www.tanzaniaweb.live