Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safaricom yawatimua wafanyakazi 28 kwa utapeli

Safaricom Kampuni ya Mawasiliano ya Safaricom nchini Kenya

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya Mawasiliano ya Safaricom nchini Kenya, imewafuta kazi wafanyakazi 28 kuanzia mwezi Machi 2021, kwa makosa ya utapeli tofauti na idadi ya mwaka 2020 ya wafanyakazi 16.

Ripoti iliyotolewa na Shirika hilo imeonesha kuwa uchunguzi ulifanyika kwa wafanyakazi 36 kwa madai ya utapeli na kubaini jumla ya wafanyakazi 28 kuhusika katika vitendo hivyo, na kutoa onyo kali kwa wafanyakzi 19 waliosalia huku kesi ya mfanyakazi mmoja ikifikishwa katika ngazi ya Serikali kwa ajili ya hatua za kisheria.

Aidha ripoti hiyo imebaini kuwa jumla ya kesi 22 zilihusisha udukuzi wa mawasiliano kwa watumiaji wa mtandao huo huku kesi 8 zikiwa ni za kwenda kinyume na maadili ya kazi , na kesi 2 zikiwa ni za matumizi mabaya ya mali za ofisi.

Shirika hilo limesema kuwa tayari limeanzisha kitengo maalum cha kusimamia masuala yote ya utapeli, uchambuzi yakinifu wa wateja, kufatilia usalama wa taarifa za mteja pamoja na kutoa elimu juu ya vitendo vya utapeli unaofanywa kwa njia za kimtandao.

" Kikosi cha kusimamia suala hili tayari kimeshakamlika katika maeneo makuu matatu, kwa maana ya kuwabaini wateja wasio na usajili kamili, kuongeza uelewa kwa wateja katika suala hili, pamoja na kufatilia kwa ukaribu maduka yote yanayouza laini za mtandao wetu" imesema ripoti hiyo.

Suala la udhibiti wa udukuzi wa mawasiliano limepewa kipaumbele mara baada ya Serikali nchini humo kuweka taratibu mpya zinazozitaka kampuni zote za simu kuhakikisha zinatunza taarifa za wateja na endapo kutatokea malalamiko juu ya udukuzi basi kampuni husika itapigwa faini ya Ksh milioni 5 sawa na Tsh bilioni 100.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live